Waziri wa Utamaduni awatolea uvivu wasanii Bongo Muvi

Wednesday July 11 2018

 

By Rhobi Chacha

Zanzibar. Waziri wa Habari Utamaduni na Mambo ya Kale Zanzibar, Mahmood Thabith  Kombo  amesikitishwa na wasanii wazawa kutojitokeza kwa wingi katika soko la filamu lililozinduliwa leo Jumatano mjini Zanzibar na Discop (Gurio).

Mahmood amesema katika uzinduzi huo wamejaa wasanii wa Nigeria, Ethiopia, Kenya na wa Afrika Magharibi wakati jambo hilo linafanyika Tanzania.

Amesema Watanzania wachache hata Wakenya na Waganda wametuzidi na hatarajii kusikia wasanii wa Tanzaniai wakilalamika kuwa hawakuwa na taarifa, huku akihoji kama hilo likijitokeza je nchi zingine wamepataje taarifa.

Aidha amesema wasanii wa Kitanzania wamekuwa nyuma kuchangamkia fursa, huku wakiwa ndio wa kwanza kulalamikia serikali kuwa hawawapi fursa wala majukwaa ya kimataifa ili kutangaza kutangaza kazi zao.

Aidha amesema Discop ni mara ya kwanza kushiriki tamasha la ZIFF, na ndio uliowasaidia Hollywood na Bollywood kunyanyuka katika soko la filamu,hivyo kama wakitaka Bongowood na Zollywood basi wachangamke.

Advertisement