Wasanii Chadema wapeta kura za maoni

Thursday July 16 2020

 

By Nasra Abdallah

Wasanii waliochukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamepeta katika uchaguzi wa chama wa ndani.

Wasanii hao ni Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa J.

Sugu anatetea kiti chake katika Jimbo la Mbeya Mjini ambapo ameliongoza kwa vipindi viwili mfululizo, Profesa Jay yeye anatetea kiti chake Jimbo la Mikumi ambalo kaliongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Katika kura hizo za maoni Sugu amepata kura za ndio 294 na hapana tano huku Profesa Jay akipata kura 137 za ndio na moja ikiharibika.

Katika kurasa zao za Instagram kwa nyakati tofauti wameonyesha kufarahishwa na matokeo hayo ambapo Sugu aliandika “Asante sana mkutano mkuu wa Chadema jimbo la Mbeya Mjini kwa kuniamini tena, Kura za  ndio 294 na hapana tano mlizopiga ni heshima na imani kubwa sana kwangu. Sasa tukutane kwenye kampeni”

Profesa Jay ameandika “Asante sana Mwenyezi Mungu, asanteni sana wana chadema wa jimbo la mikumi kwa kuendelea kuwa na imani kubwa sana nami, hili ni deni kubwa sana mmenipa leo nawaahidi sitawaangusha Mikumi Stand Up”.

Advertisement

Advertisement