Wasanii Bongo Movi kufanya Tamasha Iringa

Tuesday April 10 2018

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Waigizaji wa filamu nchini Tanzania wamewataka vijana kujiajiri na kufanya kazi kwa bidii na siyo kubweteka na kukaa vijiweni kusubiri kuajiriwa.

Akizungumza na MCL Digital kwenye kikao hicho kilichofanyika leo katika bar ya Break Point Kinondoni Jiji Dar es Salaam, mmoja wa wasanii hao Johari Chagula amesema wasanii baadhi wameamua kufanya Tamasha Jumamosi ya wiki hii Iringa Mjini Mwembe Tongwa, lengo la mkutano huo ni kutaka Kuelimisha vijana wa Iringa waamke wafanye kazi watoke kijiweni.

Aidha Johari alisema, katika Tamasha hilo hakutakuwa na kiingilio, kwani wanataka vijana wengi wajitokeze kupata elimu hiyo.

Katika kikao hicho cha leo wasanii waliohudhuria ni Johari, Shamsa Ford, JB, Mayasa Mrisho, Aunt Ezekiel, Tausi.