V-Money, Rotimi mapenzi kama yote

Muktasari:

Money alikuwa na mahusino ya kimapenzi kwa muda mrefu na msanii mwenzake wa Bongo, Juma Jux kabla ya kuwa na Rotimi Mmarekani mwenye asili ya Nigeria.

Dar es Salaam. Msanii Olurotimi Akinosho 'Rotimi' ametupa kijembe kwa kusema haachani na mpenzi wake Vanessa Mdee 'V Money'.

Rotimi aliyezaliwa Novemba 30, 1988, alisema katika kipande cha video ambacho V money amekiposti katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiiongelea miaka yake 13 ya kufanya muziki wa Bongo Fleva.

"Hatuachani," alisema Rotimi wakati huo ambao V Money alikuwa akijirekodi katika maongezi hayo huku akiwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari ya kujinginga na maambukizi ya virusi vya corona.

Wapenzi hao wapo karantini na baada ya kufanya muziki V Money kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na mapumziko anakitumikia kipindi hiki kuwa na mapumziko kifurahia maisha na mapenzi wake huyo.

"Najivunia miaka 13 niliyonayo katika Bongo Fleva, nimejitahidi kufanya kile ambacho roho inapenda, nimepata pia mpenzi ambaye amenifanya kuendelea kufurahia maisha. Asante kwa sapoti.

"Hiki kipindi tunapaswa kukitumia kujipatanisha na Mungu ili atusaidie katika janga hili la corona," alisema V money ambaye alizaliwa mwaka mmoja na mpenzi wake.

Mbali na kuwa mpenzi wa V money ni msanii wa muziki mwenye albam tano ambazo ni The Beauty of Becoming, Jeep Music, Vol. 1, The Resume, Walk with Me.

Muigizaji Rotimi amepata katika tamthilia ya Boss akiwa kama Darius Morrison na Andre Coleman katika  Power. Muvi yake ijayo inaitwa Coming 2 America bado haijatoka.