Ukimfanyia haya mwanamke atakupenda milele

Baadhi ya wanaume wamekuwa wakiumiza vichwa watafanya nini kuwaridhisha wenza wao waendelee kuwa mioyoni mwao.

 

IN SUMMARY

  • Yapo mambo mengi ya kuwaridhisha, lakini kama kesi ni kuwaridhisha kimahaba ukiachilia faragha, mambo haya matano ni matamu kama sukari maishani mwao.

Advertisement

Baadhi ya wanaume wamekuwa wakiumiza vichwa watafanya nini kuwaridhisha wenza wao waendelee kuwa mioyoni mwao.

Yapo mambo mengi ya kuwaridhisha, lakini kama kesi ni kuwaridhisha kimahaba ukiachilia faragha, mambo haya matano ni matamu kama sukari maishani mwao.

MSIFIE UZURI WAKE

Katika maisha yako kumbuka kuwa mwanamke kwa kawaida hupenda kusifiwa. Hata mtoto mdogo wa kike ukimsifia utamuona anavyofurahi na pengine kuringa kidogo.

Hivyo tumia silaha hii ya kumsifia kila mara na kupambanua ni kiasi ni mrembo na anakuvutia kila kukicha.

Ukimwambia yeye ni mzuri na anakuvutia unamjengea kujiamini mbele yako na ataamini ni mwanamume unayemthamini.

MUONYESHE MAPENZI

Jitahidi kadri unapopata nafasi kumweleza ni kwa kiasi gani unampenda. Unaweza kufanya hivi hata kwa ujumbe mfupi wa maandishi, wanawake pia hupenda kusikia wanaume walio nao wanawapenda kiasi gani.

Haiwezi kuwa kila siku au kila mwezi, bali unapokumbuka kufanya hivyo jitahidi ufanye, hili litamfanya aamini uhusiano wenu ni kutoka moyoni.

MLINDE VYEMA

...Angalia usipite hapo

...Itabidi uchukue gari (kama hana), muda umekwenda sana njia siyo salama kwako.

Hayo ni maneno ya faraja anayopenda kusikia mwanamke na kuamini kuwa mwenza wake anajali kuhusu usalama wake. Uwe mwepesi pia mnapotembea kumdaka iwapo atakanyaga jiwe au kutaka kudondoka kimahaba, usijisahau hilo ni jukumu lako.

MUONYESHE NI WAKO

Ukitoka naye usikae mbali wala kuogopa kumkumbatia au kumbusu mbele za watu. Mkiwa pamoja na marafiki anahitaji ufanye vitu (siyo vya aibu), kuonyesha wewe ni wake, kumshika mkono, kumbusu, kumkumbatia, kumshirikisha na hata kumtolea mifano mizuri.

VITU MUHIMU KWAKE

Kuna ambao wanasamehewa makosa yao makubwa kwenye uhusiano kwa sababu wana kumbuka sana siku za kuzaliwa wenza wao. Hakikisha husahau matukio yake muhimu kama siku ya kuzaliwa, alipohitimu masomo yake, aliajiriwa lini.

Hapa usisahau vitu anavyopenda viwe vyakula, maua, nguzo na ukipata nafasi ya kifedha siku moja moja uwe unamnunulia kwa kumshtukiza.

Atakuona ni wa thamani kwa sababu unakumbuka anavyovikumbuka na kuvipenda, hakikisha unakuwa wa kwanza kumkumbusha. Tukutane wiki ijayo

More From Mwanaspoti
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept