Tanasha aonyesha tarehe halisi ya mtoto kuzaliwa

Tuesday October 8 2019

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. “Nimekaa leba kwa saa 17 na ujauzito wangu umedumu kwa wiki 42, nimejifungua kwa njia ya kawaida, sasa ni mama wa mtoto mzuri wa kiume anayeshea ‘birthday’ na mpenzi wangu (Diamond),” aliandika Tanasha.

Hayo ni maandishi ya Tanasha aliyatumia kuandika Insta Stories yake juzi na kuweka kibandiko maalum cha Hospitali ya Aga Khan jijini Dar alichovishwa mkononi kikionesha mtoto wake amezaliwa Oktoba 2, mwaka huu na namba ya kuzaliwa ni 158-03-1.

Hii ni katika kuweka mambo sawa kutokana na baadhi ya mashabiki huko mitandaoni kudai mtoto huyo amezaliwa muda wa wiki nne zilizopita. Hivyo waliwajia juu familia ya Diamond na kutaka waache kudanganya watu tarehe husika ya kuzaliwa mtoto.

Diamond alitangaza katika mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa amebahatika kupata mtoto wa kiume na mpenzi wake Tanasha, katika tarehe hiyo ambayo na yeye amezaliwa. Baada ua muda akaja kuandika dada wa Diamond, Esma Platinum na Mama Diamond, Sadra.

Advertisement