Snura wala hana taimu

Tuesday September 11 2018

 

MWANADADA mkali wa filamu anayekimbiza pia kwenye muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi, amesema hana muda wa kumjadili ama kumzungumzia mtu kwani hata yeye hapendi kuzungumzwa maisha yake binafsi zaidi ya kazi zake za sanaa.

Snura alisema mtu anayemjadili na kumzungumzia maisha binafsi ama familia yake ni sawa na kumuingilia uhuru wake, kitu ambacho hakipendi.

“Kuna wakati mtu anaangalia kazi yake kumwandika mtu habari ambayo hana uhakika nayo bila kujua inaweza kuleta tatizo kwa mhusika, naumia sana na kuna wakati tunaingizana kwenye majanga, tuoneane huruma,” alisema Snura.

Staa huyo wa Majanga, Chura na nyimbo nyingtine alisema anapenda mtu aongelee kazi yake ya sanaa muziki na uigizaji kwani ndio kitu anachotamani kijulikane kwa mashabiki wake na si maisha yake binafsi ambayo si muhimu sana kuanikwa.

“Maisha yangu binafsi sio ishu wala kuwa na faida kwa jamii, ndio maana sipendi kabisa wanaonifuatilia maisha yangu, mi simfuatilii mtu.”

Advertisement