Si rahisi kusaidiwa na mtu

Muktasari:

  • Mwigizaji JB anasema anaishukuru kazi yake ya uigizaji kwani inampatia kazi nje ya uigizaji na kuingiza fedha kwa kutumia jina lake vizuri, maslahi hayo yanatokana na kuwa balozi wa makapuni kadhaa.

JACOB Stephen ‘JB’ mwigizaji nguli katika tasnia ya filamu Bongo anasema katika maisha si rahisi kusaidiwa na mtu mnayefanana katika shughuli, JB anasema hata kama atakuwa na nafasi ya kufanya hivyo hatuweza kufanya hivyo kwasababu ni mshindani wake.

“Si rahisi kusaidiwa na mtu ambaye unafanya naye kazi hata akiona umefanya jambo nzuri atajifanya hajaona kwa sababu akikusifia tu, tayari utakuwa umemshinda na kuwa juu yake kitu ambacho siyo,” alisema JB.

Jb anasema anaishukuru kazi yake ya uigizaji kwani inampatia kazi nje za uigizaji na kuingiza fedha kwa kutumia jina lake vizuri, maslahi hayo yanatokana na kuwa balozi wa makapuni kadhaa lakini pia jina lake limpata faida anapoingia katika biashara na watu tofauti kutokana na utendaji wake mzuri na uaminifu.