Shilole anataka kazi na siyo kiki

Tuesday April 2 2019

 

By Olipa Assa

MWANADADA mjasiriamali na msanii wa muziki na filamu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesema ameamua kujitofautisha na mastaa wengine kwa kufanya shuguli zake bila kiki.

Shilole anasema anaamini katika kujituma na kutumia fursa za nafasi aliopo kwamba ndivyo vinavyomfanya maisha yake yastawi kila siku.

"Sipendi kuishi maisha feki, ndio maana unaona napambana kwa kadri ninavyoweza ili kutengeneza maisha yangu halisia, Shilole awe ni yuleyule mahali popote nitakapokutana na watu.

"Muda wangu naupangilia vizuri kufanya biashara ya chakula, muziki pia kumtunza mume wangu na ndio maana unaweza kukuta naisha naye kwa amani siku zote.

"Awali wengi walikuwa wanajaji kwa nini Shilole ameolewa na mtu ambaye sio maarufu, unajua ndoa ni kitu kikubwa, nilihitaji mtu ambaye ni mwelewa na mpambanaji ndivyo alivyo ninayeishi naye,"anasema.

 

Advertisement