Breaking News
 

Shilole: Nyi’ shangaeni lakini ndiyo hivyo

Friday December 29 2017

 

KAMA una wasiwasi na mwenza wako hiyo ni wewe, lakini Diva wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, anamwamini mume wake kwa asilimia moja na kama utampelekea umbea utajisumbua tu.

Shilole anasema kwa mahaba anayopewa na mumewe huyo, Uchebe, hana wasiwasi kama labda atakuwa na mwanamke mwingine zaidi yake.

Shilole aliyefunga ndoa na Uchebe hivi karibuni, anasema japo watu watamshangaa kwa jauli hiyo, lakini ndiyo ukweli kwani kwa anavyomjua Uchebe hawezi kuwa na mwanamke mwingine nje.

Mwanadada huyo mzaliwa wa Tabora anasema ameshamwekea mumewe mitego mingi, lakini hakufanikiwa kumnasa hata mara moja hivyo anachofanya kwa sasa ni kuzidisha mapenzi ili ndoa yao idumu muda mrefu.

“Sijarogwa hata, nasema haya nikiwa na akili timamu. Mume wangu Uchebe hana mchepuko, yaani niko peke yangu, ndio maana watu wanamuona kama kadata kwangu ila wajue hayo yote ni mapenzi ya dhati anayonionyesha,”alisema Shilole aliyewahi kutoka na Nuh Mziwanda. Amedai pia yuko tayari kupambana na waliozoea kung’ang’ania waume za watu.