Saleh Kupaza arejea Twanga

Friday February 14 2020

Saleh Kupaza arejea Twanga,MUIMBAJI ,mtunzi wa muziki wa dansi, Salehe ,i The African Stars ‘Twanga Pepeta’,

 

By Rhobi Chacha

MUIMBAJI na mtunzi wa muziki wa dansi, Salehe Kupaza amerejea katika bendi yake ya zamani The African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Bendi hiyo, Hasan Rehani amesema, Kupaza amerejea Twanga wiki hii ikiwa ni miaka 10 tangu ajiengue mwaka 2010, na tayari ameshaanza kutunga nyimbo ambazo zitatambulishwa hivi karibuni kwa mashabiki wa muziki huo.

“Kupaza amerudi nyumbani, tumeona hakuna namna ya kumkatalia kurudi sababu tunatambua mchango wake katika bendi ya Twanga Pepeta na hivi navyokwambia tayari ameshaanza kutunga nyimbo ambazo ataziachia hivi karibuni kwa masha-biki wa muziki wa dansi,” alisema Rehani.

Kupaza mwaka 2015 alijiunga na bendi ya Double M Puls chini ya Muunin Mwinjuma ambako hata hivyo hakukaa muda mrefu akahama na kuanzisha bendi iliyokuwa inaitwa Ivory akiwa na wanamuziki Ramadhani Pentagone na Dogo Rama na baadaye bendi hiyo ilikuja kuvunjika.

Advertisement