Rose Ndauka msimchukulie poa jamani

Tuesday December 5 2017

 

KAMA ulikuwa unamchukulia poa, mwigizaji Rose Ndauka, pole yako. Kimwana huyo yupo makini sana na ameusoma mchezo ulivyo kwenye tasnia ya sanaa na kuamua kujiongeza.

Rose alisema maisha yana nafasi kubwa kwa mwanadamu na unaposhindwa kufanya hivyo lolote linaweza kutokea, ndiyo maana amekuwa mjanja kuangalia njia nyingine za kujikwamua mapema ili asiaibike.

“Maisha yana nafasi nyingi za kukufanya ufanikiwe ili ndoto zako zitimie, mtu asipende kung’ang’ania vitu vinavyokutesa na kukuumiza na kuna uwezekano mkubwa unazuia mafanikio kuja kwako kizembe,” alisema Rose.

Rose alisema amekuwa na utamaduni wa kupenda kuangalia fursa ilipo na kuchangamkia na sasa licha ya kuendelea kukomaa na uigizaji, pia anafanya shughuli zake za ujasiriamali.

“Sijabweteka na uigizaji tu, nachakarika kwenye ujasiriamali ili maisha yaende, unajua maisha ni kuchagua, wasanii wenzangu na wengine wasing’anganie kitu kimoja,” alisema Rose.