Riyama kuelimisha jamii kuhusu corona

Friday April 3 2020

 

By Olipa Assa

MSANII wa filamu nchini, Riyama Ally amesema atatumia umaarufu wake kuelimisha jamii namna ya kujikinga na corona.
Amesema kipindi hiki ni kigumu ambacho licha ya kuzingatia ushauri wa kitabibu pia anaona ni wakati wa kukaa sawa na Mungu.
"Tuendelee kuzingatia kile tunachoambiwa na wataalamu wa afya, lengo ni kuhakikisha hivyo virusi vya corona havisambai,"
"Nje na hilo kuna haja ya kumuomba Mungu ili kutuepusha na hili janga, kila mtu kwa imani yake naamini atasikia,"anasema.
Mbali na hilo amesema kumekuwa na changamoto ya kufanya kazi zao kutokana na kuepuka misongamano inayokatazwa na serikali.
"Nia ya serikali kutuambia tuepuke misongamano ni njema kwani inalenga kuepusha hivyo virusi visisambae na liweze kumalizika haraka ili tuendelee na shuguli zetu,"amesema.

Advertisement