Rapa Khaligraph Jones aibeba Afrika Mashariki

Muktasari:

  • Kwenye orodha ya rapa bora Afrika kwa mwaka 2018 katika nchi za Afrika Mashariki, ametajwa peke yake.

Rapa Khaligraph Jones kutoka Kenya ametajwa katika orodha ya wasanii bora wa Hip Hop Afrika wa mwaka 2018.

Msanii huyo ametajwa katika jarida la Tina ambapo Nasty C kutoka Afrika kusini anashika nafasi ya kwanza.

Kwa mujibu wa jarida hilo, rapa huyo anashika nafasi ya saba akiwakilisha Afrika Mashariki.

Kwenye orodha ya rapa bora Afrika kwa mwaka 2018 katika nchi za Afrika Mashariki, ametajwa peke yake.

Rapa pekee wa kike aliyebahatika kupenya kwenye orodha hiyo ni Nadia Nakai akiiwakilisha Afrika Kusini.