Pulev alimwa faini kisa busu

Thursday May 23 2019

 

By Thomas Matiko

BOKSA wa uzani wa Heavyweight, mpinzani wa Antony Joshua, Kubrat Pulev ambaye ni raia wa Bulgaria kaamrishwa kuingia kwenye darasa za ushauri nasaha baada ya kumpiga busu la ghafla na kumshika makalio yake mwanahabari wa kike kipindi akiwa anamhoji.

Aidha katakiwa kulipa faini ya Dola 2,5000 (Sh250,00) kwa kitendo hicho cha kumdhalilisha mwanamke huku akipigwa marufuku ya kujihusisha na ndondi hadi Julai mwaka huu.

Pulev mwenye miaka 38, alimpiga mate mwanahabari Jennifer Ravalo mwezi Machi wakati akimfanyia mahojiano baada ya pambano lake mjini California, Marekani.

Kitendo hicho kilimkwaza Ravalo aliyeshindwa kuendelea na mahojiano na wakati akiondoka, Pulev akamshika makalio yake bila ruhusa.

Ravalo alikwazika na kupitia wakili wake alisema kitendo cha boksa huyo kilikuwa cha kuudhi na kinyume na sheria, kwani hakumuomba ruhusa hiyo kwa sababu hawana mahusiano yeyote.

Naye kamishna wa michezo katika Jimbo la California, Martha Shen alisisitiza lazima Pulev aadhibiwe ili iwe funzo kwake.

Advertisement

Bondia huyo mara moja alipigwa marufuku ya kushiriki pambano lolote katika Jimbo la California mpaka pale atakapolima faini na kuingia darasa la ushauri nasaha kufikia Julai 22 mwaka huu.

kutokana na kitendo hicho, Pulev alimwomba msamaha Ravalo na kuahidi kulipa faini hiyo. Vile vile Pulev aliadai Ravalo ni mshikaji wake wa siku nyingi na alimpiga busu kutokana na furaha ya ushindi wake na sababu wanafahamiana japo hawana mahusiano.

Pulev alikuwa akihojiwa na Ravalo baada ya ushindi wa pambano lake dhidi ya Bogdab Dinu.

Pulev aliratibiwa kupambana na Joshua 2017 ila akajiondoa baada ya kupatwa na jeraha.

Advertisement