Penzi la Leo Mysterio labadili maisha ya Riyama

Thursday February 6 2020

Penzi la Leo Mysterio labadili maisha ya Riyama,Mcheza filamu, Riyama Ally ,mumewe Leo Mysterio,

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam.Mcheza filamu, Riyama Ally amesema maisha yake ya sasa yamebadilika kutokana na kuishi vizuri na mumewe Leo Mysterio.

Riyama amesema anakerwa na maneno ya watu mitandaoni kwamba anamtawala Leo Mysterio, wakati ukweli ni kwamba wanaishi kwa kusikilizana.

“Watu wanaongea sana uzushi, kitu ambacho mimi kinaniumiza. Leo Mysterio hakuwa hivi, mimi ndiye nimemuweka katika maisha tofauti na ushauri wangu ameufuata, sina haja ya kufafanua ila Leo Mysterio wa sasa si yule wa zamani,” anasema Riyama kwa kujiamini.

Msanii huyo anasema anajisikia vizuri kuishi maisha huru na kusikilizana na mume wake, hayo mengine anawaachia ‘wanaa’ wanaohangaika kutwa, kucha na mambo ya watu.

“Mimi naona tupo vizuri, maisha yetu yanasonga. Tunashirikiana kwa kila kitu, ndio maana sioni aibu kuambiwa naishi na mwanaume niliyemzidi umri.

Riyama amefunga ndoa mwaka 2016 na mume wake Leo Mysterio.

Advertisement

Advertisement