Breaking News
 

Pastor Myamba kumbe alikuwa hatanii

Tuesday December 5 2017

 

KUMBE ile staili yake ya kuigiza ya kichungaji katika filamu alizocheza mwigizaji nyota nchini, Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ haikuwa utani, kwani jamaa kwa sasa anamiliki kanisa lake.

Pastor Myamba anamiliki kanisa hilo eneo la Kigamboni, ikiwa ni muda mrefu tangu amiliki chuo cha uigizaji kilichosaidia kuibua vipaji vipya vya sanaa nchini.

“Naamini kuigiza ni sehemu ya kuhubiria maana filamu ni njia ya kufikisha ujumbe kwa hadhira, hivyo ninaigiza, pia ni natoa huduma ya kiroho katika kanisa la The World Life Ministry kama mchungaji,” alisema .

Msanii huyo ni mmoja wa waigizaji waliobobea kuigiza kama mchungaji katika filamu za kidini tangu enzi za marehemu Steven Kanumba, kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumtabiria kuja kuwa kiongozi wa kiroho, jambo lililokuwa kweli kwa sasa.