Nyamayao anapata tabu sana

Tuesday August 7 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

UNAMKUMBUKA Nyamayao, yule mwigizaji aliyetamba sana enzi za Kaole Sanaa hasa kwa michezo ya kwenye runinga? Kumbe kwa sasa yupo China akiendelea na shughuli zake za sanaa na anakiri amekuwa akitapa tabu kila akikumbuka Tanzania.

Nyamayao ambaye majina yake kamili ni Happiness Stanslaus, alisema huwa anahisi kuna vitu vingi vinampita na kumnyima fursa ya kuvifanyia kazi au kutoa msaada kwa walengwa kutokana na umbali aliopo kwa sasa.

“Nilitamani siku yangu ya kuzaliwa nisherehekee na yatima au wanawake wenye faraja kutoka kwangu, lakini imekuwa vigumu na nimeisherehekea kikawaida tu.”

Alisema kwa sasa anafanya kazi kwa nguvu ili akirudi Bongo aanzishe taasisi ya kusaidia jamii kama sehemu ya kurudisha shukrani zake kwao kwa kumuunga mkono tangu alipoibukia kwenye uigizaji miaka ya 2000.