Nandy amfunika Billnass

Monday October 26 2020
billnas nandy pic

Rapa William Lyimo maarufu Billnass ambaye pia ni mchumba wa mwanamuziki Nandy amefunguka kwamba mpenzi wake anaingiza pesa zaidi yake.

Billnas ambaye Aprili 10 alimvisha Nandy pete ya uchumba wakiwa jukwaani kwenye shoo, amefunguka hayo leo Oktoba 26 wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha redio Clouds akiwa na Nandy.

Akijibu swali aliloulizwa la nani kati yao anaingiza pesa zaidi Billnass alijibu kuwa ni Nandy lakini akaenda mbali na kufafanua kuwa hata hivyo yeye ndiye mwenye pesa nyingi zaidi ya Nandy.

“Nandy anaingiza pesa zaidi yangu, anapata shows nyingi na ana miradi mingi. Lakini mwisho wa siku tukiwa tunafanya tathimini za nani ana pesa nyingi kwenye akaunti, mimi ndo nakuwa juu.”

Billnas ameeleza kwamba hiyo ni kwa sababu Nandy ana matatumizi mengi kuliko yeye, kwahiyo huingiza pesa nyingi lakini pia hutumia pesa nyingi zaidi.

Wawili hawa wamekuwa kwenye uhusuni kwa muda mrefu, uhusiano uliopewa jina la BillNandy kwenye mitandao ya kijamii na wiki iliyopita waliachia wimbo wa pamoja unaoitwa Do Me, ukiwa ni wimbo wao kushirikiana; wa kwanza unaitwa Bugana, ulitoka Agosti 2019.

Advertisement
Advertisement