Advertisement

Nabii Mswahili ana vituko nyie

MADEBE Lidai ‘Nabii Mswahili’ ana vituko sana, kwani jamaa amesisitiza yeye ni mzalendo na anaipenda lugha yake ya Kiswahili, hivyo juzi kati aliamua kuigoma kampuni moja (jina kapuni) kwa sababu mkataba uliandikwa Kiingereza.

IN SUMMARY

Alisema aliugomea kwa kutaka uandikishwe kwa Kiswahili kwa vile alioingia nao na yeye wote ni Watanzania ambao Lugha ya mawasiliano ni Kiswahili, hivyo aliona ni muhimu kuienzi lugha hiyo ili mkataba ueleweke kwa kila mmoja kwa ufasaha. “Niliugomea mkataba huo wa Kiingereza, sio kama sijui ila nataka watu waizoee lugha yao na kwa umuhimu wa filamu zangu jamaa walikubali,” alisema.

“Sina kingine kinachoweza kunitambulisha kama Mtanzania na Mwafrika ila lugha yangu ya Kiswahili kwa kuzingatia hilo. nilikataa kujaza mkataba huo na ikabidi utafsiriwe.” Nabii Mswahili alisema hata kwenye filamu hakuna sababu ya kuigiza na kuzipa jina kazi zinazotumia Kiswahili na kutumia mikataba ya kigeni wakati majadiliano ya kuuziana filamu yenyewe inatumika Kiswahili, ndio maana alikuwa radhi apoteze fedha, ili kutetea lugha hiyo.

More From Mwanaspoti
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept