Mzee Chilo ataka uwekezaji zaidi

Tuesday August 7 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

MKONGWE wa filamu Bongo, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo’ amesema soko la filamu nchini linahitaji uwekezaji mkubwa kwa nia ya kuijenga tasnia hiyona kuleta masilahi kwa wadau wote wakiwamo wasanii kwa ujumla.

Alisema hata nchi zilizoendelea kwenye fani hiyo Afrika na duniani kwa jumla walifanya hivyo, jambo linalohitajika kufanya kwa sasa hapa nchini badala ya kuendelea kuiendesha tasnia hiyo kwa mazoea tu.

“Tunahitaji vitu vizuri, lakini haviwezekani kwani uwekezaji wake bado upo chini hivyo kwa wadau wenye fedha waigie katika filamu kwa kujenga kumbi za sinema za Kitanzania na mengine ya kukuza sanaa yetu,” alisema.

Mwigiozaji huyo alisema pamoja na wadau kuwekeza katika uzalishaji changamoto inajitokeza katika kuuza kazi za filamu kwa watayarishaji kwa sababu mfumo wa DVD au katika runinga haufanyiki kwa ufasaha hivyo ni bora kuwa na kumbi za sinema za chini kuliko kuishia kuzindua tu katika kumbi zilizopo.