Mvinyo kiungo bomba kwa urembo

Tuesday May 14 2019

 

By Pauline Ongaji

Mbali na kutumika kama kinywaji, mvinyo mweupe hutumika pia katika shughuli nyingi hasa jikoni.

Lakini je, wajua kuwa pia waweza tumika kama kiungo muhimu katika masuala ya urembo? Hapa, matumizi yake ni kama yafuatayo:
Ngozi: Changanya pamoja kijiko kimoja cha chai cha mvinyo na vikombe viwili vya maji. Tumbukiza kibonge cha pamba mle ndani kisha upanguze uso wako ukishanawa kwa sabuni, kisha usisuuze. Hii itachochea mzunguko wa damu katika sehemu hii, vile vile kupunguza vinyweleo. Pia yaweza tumika kutuliza ngozi. Waweza ongeza kiwango kidogo cha mvinyo mvinyo mweupe kwenye maji yako ya kuoga. Hii itasaidia kulinda ngozi yakona kuimarisha usawa wa rangi yako.
Nywele: Suuza nywele yako kwa kutumia mvinyo mweupe. Changanya mvinyo na maji na utumie mchanganyiko huo kusuuza nywele zako. Hii huondoa masalio ya bidhaa za nywele zilizorundika na hivyo kuzifanya zing’ae. Pia, bidhaa hii ni kitulizo. Tumbukiza pamba kwenye mvinyo mweupe kisha uitumie kupangusa sehemu zilizoathiriwa na uvimbe huu na uache kwa dakika tano kabla ya kusuuza kwa maji safi na kukausha. Hii itasaidia kutuliza ngozi inayowasha na kuifanya iwe nyepesi.
Kitulizo cha mba: Changanya viwango sawa vya mvinyo mweupe na maji kisha utumie mchanganyiko huu kusugua ngozi ya kichwa na nywele zako. Pia waweza changanya kijiiko cha chai cha mvinyo mweupe kwenye shampoo yako ya kawaida na utumie kuosha nywele zako.
Miyale ya jua: Bidhaa hii husaidia kurejesha usawa wa kiwango cha pH kwenye ngozi yako. Changanya mvinyo na maji kisha utumbukize kitambaa mle ndani na utumie kupanguza maeneo yaliyochomeka kutokana na miyale ya jua.

Advertisement