Muumin arudi na albamu mpya Double M

Monday November 19 2018

 

MWANAMUZIKI wa siku nyingi katika dansi, Mwinjuma Muumin amesema atatoa albamu mwezi wa tatu baada ya kuirudisha bendi yake ya Double M.

Muumini alisema, Bendi ya Double M imerudishwa katika ulimwengu wa muziki wa dansi mwaka 2013 lakini haijatoa albamu, zaidi ya kurekodi nyimbo na kuimbwa majukwaani.

Muumini ametoa sababu ya kutotoa albamu ni kutokana na kushuka kwa soko, kwa maana unatakiwa kuuza CD, na Wahindi waliokuwa wananunua CD sasa hivi hawanunui kutokana na kwa kuingia uwoga wa wajanja.

Hata hivyo, alisema, wajanja hao wamesababisha watu wanashindwa kununua CD ya Sh5,000 badala yake wanaenda na flash katika kompyuta kuchukua nyimbo nane kwa Sh1,000 ndio maana ameamua kutumie njia mbadala ya kuuza CD zao kwenye maonyesho yao.

Mbali na hayo, Muumin alizungumzia kuchipukia kwa bendi nyingi za muziki wa dansi hivi sasa kuwa ni changamoto mojawapo ya kuurudisha muziki huo.

Advertisement