Mlela bwana, eti hajaona wa kumuoa!

Tuesday September 11 2018

 

KUMBE Yusuf Mlela naye ana vijembe? Nyota huyo wa filamu nchini, amefichua eti hajaoa mpaka sasa kwa vile hajaona mke wa kufunga naye pingu za maisha, huku akidai kwa kuwa anajua ndoa ni ibada, hawezi kukurukupa kulifanya jambo hilo bila umakini kwani asingependa aoe kisha aje kuitengana na mwenza wake.

“Suala la kuoa si kitu ambacho unatakiwa mtu ukurupuke, ni jambo muhimu na unatakiwa ujipange na kumpata mwenzako atakayeishi nawe kwa upendo na niseme wazi hadi sasa bado sijapata mwanamke anayestaili kwangu,” alisema.

Mlela anaamini mtu hatakiwi kuoa kwa sababu ya umri au sherehe kufanyika kwa kifahari bali atambue kuna maisha baada ya sherehe burudani, hivyo ni vema kuchagua mtu atakayevumiliana naye kwa kila hali kama mke na mume kwa upendo.

Advertisement