Mjue mimi ni kama Samatta vile- Ray

Tuesday November 20 2018

 

NGULI katika tasnia ya filamu Bongo movie Vincent Kigosi ‘Ray’ ametamba kuwa anajivunia kuwa msanii pekee kwenda nje ya nchi kurekodi filamu hasa kwa wakati huu ambao wengi wanalia wakisema soko si rafiki kwa watayarishaji wa filamu.

“Mimi kama Samatta vile nimemua kwenda kutengeneza filamu nchi za nje kwa maana moja kuu kuweza kutengeneza mashabiki nje ya mipaka ya Tanzania na kuwa wa kimataifa,”alisema Ray.

Ray anasema kuwa kuna sinema ambayo ameigiza kama mchezaji mpira wa kulipwa kutoka Tanzania na kucheza mpira nchini Zambia, lakini kuna filamu nyingine ambayo ameigiza nchini Afrika ya Kusini, kwa mantiki hiyo kazi zake nyingi atakuwa akirekodia nje ya nchi.

Advertisement