Mazishi ya mke wa P Diddy noma!

Monday November 26 2018

 

JUZI Jumamosi ilikuwa siku ngumu kwa rapa maarufu na mwenye pesa ndefu duniani, Sean Combs a.k.a P Diddy pamoja na watoto wake, wakati akishughudia jeneza lenye mwili wa mke wake, Kim Porter likishushwa ndani ya kaburi.

Mazishi ya Kim Porter yamefanyika juzi Jumamosi kwenye makaburi ya Evergreen Memorial Park Mjini Georgia ambako, mastaa kibao walihudhuria.

Hata hivyo, Diddy muda mwingi alionekana akiwa amekaa jirani na kaburi hilo la mkewe wa zamani wakati waombolezaji wengine wakiendelea na zoezi la kufyatua fataki.

Kivutio zaidi kwenye mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mastaa wa nguvu akiwemo Usher Raymond, Mary J. Blige, Dallas Austin, Ebony Electra, Marvett Britto, Diddy na Quincy Brown ambao walikuwa kivutio kwa waombolezaji wengine.

Lakini, macho ya wengi yalikuwa kwenye jeneza lililohifadhi mwili wa Kim, ambapo lilikuwa limenakshiwa kwa dhahabu hukumara nyingi Diddy alikuwa akionekana kuwa pembeni.

Kim alizikwa pembeni ya kaburi la mama yake, Sarah Lee Porter aliyefariki mwaka 2014, wakati Diddy alitumia muda mwingi akiwa kwenye eneo hilo peke yake huku akiwa mwenye huzuni na wakati mwingine watoto wake akiwemo, Christina Combs walijumuika naye.

Advertisement

Baadaye Diddy aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akimwelezea Kim kuwa, alikuwa mfano wa mama bora hapa duniani.

Jeneza la Kim mbali na kunakshiwa kwa dhahabu, pia lilipambwa na maua ya kila aina huku moja ya picha yake ambayo ilikuwa ikipendwa sana na mashabiki ikiwa pembeni.

Kwaya iliyokuwa ikitoa burudani kwenye mazishi hayo ilikuwa kivutio cha aina yake kutokana na vyombo na sare za wanamuziki wote kunakishiwa kwa rangi nyeusi na nyeupe.

Miongoni mwa wanamuziki waliopanda jukwaani kumsindikiza Kim kwenye safari yake ya mwisho ni Faith Evans, ambaye ni mke wa zamani wa swahiba wa P Diddy, Notoriuos BIG aliyeimba wimbo wa His Eye is On the Sparrow wakati Yolanda Adams naye hakuwa nyuma kutoa neno.

Advertisement