Maua Sama na Kiba imekaaje?

Friday November 15 2019

Maua -Sama - Kiba- kwani -vipi-wasanii-muziki-ngama-mashabiki-burudani-

 

By Rhobi Chacha

SUPASTAA wa kike wa Bongo Fleva, Maua Sama amefunguka kuhusu ukaribu na AliKiba, akisema wamefahamiana muda mrefu sana kabla hata hajawa maarufu.

Maua ambaye ametesa kinoma na ngoma ya Iokote, amesema AliKiba alisikia sauti yake kwenye ngoma ya ‘Hata Sielewi’ ya Mwana FA kuanzia hapo ndipo walipoanza kupendana na kuwa shabiki wake.

“Nadhani watu wanashangaa ukaribu wangu na Ali, ukweli sijaanza leo wala juzi, AliKiba alianza kusikia sauti yangu kabla hata hajaniona ‘live’ na wala sikuwa najulikana. Alisikia ngoma ya Mwana FA, siku moja nilikutana naye akaniambia nina sauti nzuri akanipongeza na mimi nilimpongeza kwa kazi yake na muziki hapo ndipo nilipoanza kuwa shabiki wake na kufahamiana.

“Ilikuwa naenda nyumbani kwake nakutana na ndugu zake, tukafahamiana zaidi na kuweza kunipa ushauri katika kazi yangu,” anasimulia Maua Sama, ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ya ‘Niteke’.

“Kiukweli sikuwa nafahamu kitu kuhusu remix ya wimbo wangu Niteke, Hamornize kanifanyia ‘Sapraizi’ maana nilikuwa safari, akanipigia video call kuniomba anahitaji kufanya remix ya wimbo huo, na video call hiyo alinipigia akiwa anarekodi wimbo huo, kweli nilifurahi sana,” anasema Maua Sama.

Advertisement