Matumaini wa jana wala sio wa leo mjue

KAMA bado unaamini kuwa mchekeshaji Tumaini Martin ‘Matumaini’ bado yupo vilevile tangu alivyoibuka katika fani hiyo. Matumaini wa sasa amezaliwa upya sio kwa imani yake ya kilokole tu, bali hata mfumo wa maisha yake ya kawaida.

IN SUMMARY

Pia mkali huyo anakiri kama sio kuokoka kwake na kujitosa kwenye uimbaji wa nyimbo za Injili hajui angekuwa na hali gani, kwani fani ya filamu na tamthilia kwa sasa soko lake limesimama tofauti na ilivyokuwa enzi akitambia huko.

Advertisement

“Namshukru Mungu kwa kunionyesha njia sahihi mapema maana, kila kitu changu kwa ssa kimebadilika na sijui kama nisingeokoka na kuimba wa muziki wa Injili maisha yangu yangekuwaje na changamoto ya soko la filamu lilivyo kwa sasa.”

Matumaini aliyeibuliwa kupitia Kaole Sanaa akinoga zaidi akicheza na Kiwewe, alisema kwa sasa mbali na kuimba, lakini ni mjasiriamali na ni MC wa shughuli mbalimbali akitengeneza noti.

More From Mwanaspoti
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept