Mama kubwa:Ni watu wawili tofauti kabisa

Muktasari:

  • Mariam ametamba katika tamthilia Mama Kubwa, Jesca, jirani na filamu kibao.

MARIAM Ismail mwigizaji wa filamu Bongo movie anasema kuwa uhusika ambao aliwahi kuigiza na kuonekana kama mwanamke mbabe na asiyependa kubabaishwa ni uhusika wa filamu tu, yeye ni mtu ambaye anaheshimu wanaume na kubaki nafasi yake kama mke.

“Unapokuwa msanii lazima uendane na uhusika unaopewa katika, tamthilia ya ‘Mama kubwa’ ambayo ndio jina nililotumia nilioneka kama mbabe lakini sipo hivyo ni mpole na nasikiliza watu,” alisema Mariam.

Mama kubwa anasema pamoja na kuwa msanii mkubwa lakini katika tasnia ya filamu kuna changamoto nyingi hasa unapokutana na mwigizaji unayemzidi kiwango katika uigizaji.

Mariam ametamba katika tamthilia Mama Kubwa, Jesca, jirani na filamu kibao.