Maisha ni mapito Lulu

Tuesday November 20 2018

 

MWIGIZAJI wa filamu nyota Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa katika maisha kila hatua mwanadamu apitayo ni sehemu ya kujifunza na kukomaa kuwa na hekima na busara hivyo haitakiwi kukata tamaa kwa kila upatapo changamoto.

“Maisha ni sehemu ya mapito kuna wakati unaweza kukata tamaa kama hauna Mungu lakini unapokuwa na imani na unamwamini Mungu unapata ujasiri na kusimama imara,”alisema.

Lulu anasema kuwa moja ya jambo ambalo amewahi kujifunza ni kuwasikiliza wazazi wanapokushauri kwani kwa hali yoyote ile wanajua mengi ambayo kuna wakati si rahisi kwa mtoto kuyatambua yapi ni busara kutenda yeye amekua na anatarajia kuwa mfano bora kwa jamii.

Advertisement