Kwa muziki huu, mtaikoma Bogoss

Monday November 19 2018

 

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Bogoss Musica, iliyo chini ya Nyoshi El Saadat ‘Rais wa Milele’ wiki iliyopita imepata vyombo vipya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nyoshi alisema, vyombo hivyo ni vya kisasa, vikiwa na uwezo wa kumudu kutumika eneo la wazi au ukumbini, ili kuwapa usikivu mzuri mashabiki wake, huku vikingine vikitumika katika studio ya bendi hiyo iliyopo Kinondoni Manyanya.

Vyombo hivyo ni magitaa, drums, maiki pamoja na vyombo tofauti vya kuwezesha kupata muziki mzuri. Nyoshi alisema, vyombo vingine vinaingia wiki ijayo pamoja na mixer ambapbaadhi vitaanza kufanya kazi katika shoo yao ya Ijumaa katika Ukumbi wa Meridian.

“Tumeamua kuleta vyombo vipya, kwa ajili ya kuleta mwonekano mpya kwenye dansi na ukizingatia tuna studio, bado kukamilisha baadhi ya vitu ili ifanye kazi, kwa kweli tumedhamilia kufanya mapinduzi katika muziki wa dansi,” alisema Nyoshi aliyewahi kutamba na FM Academia.

Advertisement