Kwa Bill Nas! Wanakuja wenyewe tu

Monday October 29 2018

 

By Rhobi Chacha

ACHANA na ishu zingine, ambazo unazijua wewe, lakini ukweli ni kuwa William Lyimo a.k.a Bill Nas au Bill Mwenga ni miongoni mwa mastaa wanaosongesha Bongo Flava kinomanoma.

Ngoma zake kali zimekuwa zikibamba mashabiki kila kona na hasa ile staili yake ya kuimba ambayo imekuwa ikiwapa mzuka mashabiki wanapomuona jukwaani akifanya yake.

Hapa juzi kati si akakutana uso kwa uso na Mwanaspoti, ambapo akafunguka mambo flani hivi ameizingi sana kwa mashabiki wa Bongo Flava. Cheki anavyotiririka.

Mwanaspoti: Mambo vipi Bili Nas?

Bili Nas: Poa, mzima wewe?

Mwnaspoti: Niko pouwa kabisa, long time sana hatujaonana mwanangu ila leo fresh wasomaji watataka kujua kidogo una mpya gani kwenye gemu.

Bill Nas: Aaaa! Unajua kwa sasa naogopa sana media, yaani napafomu jukwaani tu au kwani vipi tukitafutana siku zingine ili nijiweke fresh kwanza?

Mwanaspoti: Acha bana ni ishu za kawaida tu kwani, umekuwa kimya kidogo kwenye gemu.

Billnas: Nipo tu, muda mwingi sana siku hizi nakuwa studio hivyo, nikiwa na kazi mpya napenda sana kutulia.

Mwanaspoti: Nilijua ndiyo yale mambo flani ya kwenye mtandao ndio umeamua kujificha.

Billnas: Hapana, mbona kipindi kilekile tu nilianza kutembea, ile ishu ni ya kawaida japo iliniumiza sana kichwa hadi kwa wazazi wangu.

Mwanaspoti: Pole sana kwa sababu ilileta noma kweli huko mitandaoni, shida ilikuwa nini?

Billnas: Tuachane na hayo, unajua sipendi kuongelea sana vitu vilivyopita, halafu havisaidii katika jamii.

Mwanaspoti: Wanamuziki wengi wanaogopa sana kuoa wanajua ndio mwisho wa muziki wao unazungumziaje hilo?

Billnas: Kwangu sidhani kama ipo hivyo, kwa sababu hilo jambo ni wajibu na lazima nilitimize hilo suala na siku si nyingi nitakualika.

Mwanaspoti: Vipi kuhusu mipango yako ya baadaye kwenye muziki?

Billnas: Baada ya miaka mitano nataka kuachana na muziki na kufanya biashara tu na muziki utabaki kuwa kwenye damu maana nina ndoto kubwa kwenye maisha yangu.

Mwana spoti: Kuna habari kuwa una bahati ya kutokewa na mademu kimapenzi, huwa inakuwaje hebu wape wana maujanja?.

Billnas: Hahaha kwanini maswali mapenzi tu? Ila mahusiano yangu mengi hayaanzagi kwenye kufukuziana, imekaa kizamani zamani sana, naanza kuwa marafiki. Unajua ukishakuwa karibu na mtu inakuwa rahisi, ile ya kuanza kufukuzia sijawahi.

Mwanaspoti: Kumbe ndio maana uliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Lina na Nandy, maana walianza kuwa marafiki zako hawa

Billnas: Hahaha kuongelea hao watu sio poa kabisa kwa sababu wana wapenzi wao kwa sasa.

Mwanaspoti: Haya asante sana.

Billnas: Shukurani.

Advertisement