Kipaji ndio shangwe kwa Riyama

Tuesday November 27 2018

 

By Myovela Mfwaisa

Nyota wa filamu nchini, Riyama Ally amefichua kudumu kwake katika fani hiyo kwa muda mrefu kumetokana na kipaji alichonacho na kumfanya awe na furaha mwanzo mwisho.

Riyama alisema anajisikia faraja kuona kipaji na ubunifu alionao umempatia mashabiki wengi kila siku, licha ya kubadilisha uhusika katika kazi na hilo linampa faraja na kuzidi kuumiza kichwa azidi kuwakomba watu.

“Ninafanya utafiti katika kuigiza uhusika wangu kwa wanaokumbuka Riyama alikuwa ni mtu wa kuigiza nafasi za huzuni na kulialia tu, lakini ghafla amekuwa mchambaji na mtu wa shombo jambo lililompa mashabiki wengi,” alisema.

Riyama alisema kwa sasa ana mikataba ambayo si wasanii wote wanafanya kazi kama yeye na amekuwa balozi wa DSTv kitu ambacho ni faida ya kipaji chake na ni furaha kubwa akizidi kujipanga ili kuwapa burudani mashabiki wake.

Advertisement