Kikosi Kazi ni ngoma juu ya ngoma

Muktasari:

Katika makundi ya muziki wa Hip Hop ambayo yanafanya vizuri hivi karibuni, kikosi kazi ni moja ya makundi hayo.

KUNDI la muziki wa Hip Hop nchini linalofahamika kwa jina la Kikosi kazi, limezidi kushika kasi hivi karibuni baada ya kuachia ngoma mbili za Anthem na Fanya Wewe kwa nyakati tofauti huku zote zikipokelewa vizuri.

 

Kundi hilo ambalo lilianza kwa kuachia wimbo wa Kazini, Sala, Fanya wewe na sasa wameachia ngoma nyingine inayoitwa jina la Anthem huku wakimshirikisha msanii Chibwa kutoka nje ya kundi hilo.

 

Kikosi kazi walianza kwa kuachia ngoma ya kazini ikiwa kama Diss Track kwa kuwajibu weusi na baada ya ngoma hiyo wakaamua kuachia ngoma mfululizo zikiambatana na video.

 

Wasanii wanaounda kundi hilo wanaongozwa na Nikki Mbishi, Stereo, One Incredible, Zaiid, Azma, Mansulii na P The Mc ambao wote wanatumia staili muziki wa kufoka foka(Hip Hop).

 

Licha ya kuanzishwa kwa kundi hili, awali wasanii hawa walikuwa wanaunda kundi la Tamaduni Music ambapo pia walikuwa wanatamba kwa kufanya vilinge kila Alhamis na walikuwa wakijikusanyia mashabiki.