Advertisement

Kalembo kashtuka mapema

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Hashir Khalfan ‘Kalembo’ amesema bila uwekezaji wa maana na bajeti nono filamu za Kibongo haziwezi kuhimili soko la kimataifa licha ya Tanzania kujaliwa vipaji vikali vya uigizaji.

 

IN SUMMARY

  • Kalembo alisema fani ya filamu haiwezi kupiga hatua kama uwekezaji na kutumia bajeti kubwa yenye kukidhi kila kitu hautakuwepo, ambao ukiungana na vipaji ni rahisi kazi za Tanzania kutamba na kuhimili ushindani anga za kimataifa.

Advertisement

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Hashir Khalfan ‘Kalembo’ amesema bila uwekezaji wa maana na bajeti nono filamu za Kibongo haziwezi kuhimili soko la kimataifa licha ya Tanzania kujaliwa vipaji vikali vya uigizaji.

Kalembo alisema fani ya filamu haiwezi kupiga hatua kama uwekezaji na kutumia bajeti kubwa yenye kukidhi kila kitu hautakuwepo, ambao ukiungana na vipaji ni rahisi kazi za Tanzania kutamba na kuhimili ushindani anga za kimataifa.

“Filamu bora inatokana na uwekezaji katika utengenezaji kama mmoja ya Wakurugenzi wa kampuni zinazozalisha kazi nchini, nimeliona hilo ndio maana tumekuwa kukitoa kazi zenye maana na usaili kwa akili klupata waigizaji mahiri.”

Kalembo anayetamba kwa sasa kupitia kampuni yake na filamu ya Sumu, alisema ukiwa na mtaji ni rahisi sana kufuatilia taratibu za uandaji wa filamu kwa kufanya usaili kupata wasanii halisi kulingana na muswada wa filamu ( Script) na si kurekodi kutoka na majina ya wasanii wanaovuma bila kujua wanaweza kuharibu kazi hiyo.

More From Mwanaspoti
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept