K2ga anaimba kama Kiba? Aaah Wapi!

KARIBU kila video ya kuimba atakayoipost K2ga, msanii kutoka lebo ya muziki ya Kings inayomilikiwa na Alikiba, huwa hazikosekani comment za masimango kwamba jamaa anaimba kwa kumuiga bosi wake King Kiba.

Mwanaspoti ilifanya mahojiano na msanii mwingine kutoka lebo hiyo, Tommy Flavour na kumuuliza mtazamo wake kuhusu ishu ya K2ga kupiga chabo kwa Kiba, Tommy amejibu;

“Sio kweli, sidhani kama anamuiga, sema inawezekana ana vitu kama vya Alikiba kwa sababu ni braza ambaye yuko karibu naye muda mwingi na anamfundi-sha vitu vingi kuhusu muziki hivyo lazima kuwe na vitu fulani vya kufanana.” alisema Tommy na akaendelea kutetea zaidi.

“Pia hakuna msanii ambaye anafanya kitu cha kwake kwa asilimia mia, wote tunakuwa inspired na wasanii wengine tunaowapenda kwahiyo kwa kesi ya K2ga naweza kusema hamuigi ila huenda kuna vitu wanafanana,” alisema Tommy.

K2ga alisajiliwa mwaka 2018 pamoja na wasanii wengine watatu, Cheed na Killy ambao kwa sasa wametimka kutoka lebo hiyo na kuelekea Konde Gang, lebo inayomilikiwa na Harmonize.