Jukwaa la Watoto lazinduliwa Ngome Kongwe

Wednesday July 11 2018

 

By Rhobi Chacha

Zanzibar. Mkuu wa Mkoa wa Mji Magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mohamed leo amezindua jukwaa la watoto katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.

Jukwaa hilo ambalo litajadili baba bora anavyotakiwa kuwa katika malezi ya watoto.

Katika uzinduzi huo umeambatana na burudani mbalimbali ikiwemo wanafunzi kucheza nyimbo za wasanii na ngongoti.

Hata hivyo, Ayoub amesema baba bora anatakiwa ajue majukumu yake kwa watoto asimuachie mama peke yake.

Pia aliongeza kusema,wapo wanaume baadhi yao wakidhani jukumu la kulea mtoto ni mama, hata shughuli za nyumbani zinazowahusu watoto wanamuachia mama peke yake.

Advertisement