Joe Boy, Wurld na Singah kuwasha moto Dar Septemba 26

Wednesday September 9 2020

 

By Nasra Abdallah

Mkali wa kibao cha Baby, Joe Boy, Wurld na Singah wa Teyamo wanatarajiwa kutua nchini  kwa ajili ya kufanya shoo.

 

Shoo hiyo ambayo imeandaliwa kampuni ya Str8up vibes itafanyika Jijini Dar es Salaam Septemba 26.

 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumatano Septemba 9,2020, Mkurugenzi wa kampuni hiyo ,Sniper Montana amesema huo  ni mwendelezo wao katika kuwapa wananchi burudani na kuiboresha.

 

Advertisement

"Pia ieleweke kwamba wasanii wa Afrika kwa sasa wamekuwa wakiangaliwa ikiwemo Tanzania,hvyo ni katika kuwaweka karibu wasanii wa Tanzania na wasanii wengine Afrika," amesema Montana.

 

Wakati Mkurugenzi wa Operesheni, Andrew Mpepo,amesema  kuhusu kiingilio na wapi show hiyo itafanyika watatangaza hapo baadaye na kueleza safari hii wamejipanga kuwapa watu wengi zaidi burudani.

 

Kwa upande wake Lilian Kanora, ambaye ni Meneja bidhaa wa Benki ya CRDB na moja ya wadhamini wa shoo hiyo, amesema wao katika shughuli hiyo watahusika katika kununua tiketi na pia kufanya matumizi kwa kuitumia kadi zao za 'TemboCard'.

Advertisement