Joao Felix apiga shoka mademu wa mtandaoni

Thursday May 16 2019

 

KINDA wa Benfica, Joao Felix ambaye msimu huu amekuwa moto wa kuotea mbali kawaomba mademu kukoma kumtongoza kwa kumtumia picha zao za uchi kwa sababu hana mpango wa kudeti kwa sasa.

Felix mwenye miaka 19, amekuwa habari za mjini msimu huu kutokana na yeye kuonyesha kiwango hasa katika michuano ya Europa.

Huku klabu kadhaa kubwa zikiendelea kummeza mate zikipambana kumsajili, Felix naye yupo bize akipambana na hali yake kikubwa zaidi ikiwa ni ishu ya mademu.

Tangu jina lake lianze kuangaziwa, amekuwa akipokea meseji kibao kwenye akaunti zake za kijamii kutoka kwa mademu wanaomtongoza huku wengi wakiamua kumshawishi kwa kumtupia picha zao za uchi.

Hata hivyo, Felix kawapiga shoka kwa kuwaambia wanajisumbua kwa kuwa hana muda kabisa na mademu kwa sasa.

“Bwana sijawazia kabisa kusaka demu, mimi bado mdogo sana na kila kitu kina wakati wake, kwa sasa nawaza soka tu, ikifika muda basi nitalifanyia kazi hivyo wasijisumbue kujaribu kunizengua,” Felix kanukuliwa.

Advertisement