Rodriguez amchanganya Jennifer Lopez

Saturday November 25 2017

 

New York, Marekani. Jennifer Lopez ‘J-Lo’ amenogewa na penzi la Alex Rodriguez tangu walipoanza uhusiano Februari.
Kwa mara ya kwanza Jennifer amesema katika maisha yake ya uhusiano, hakuwahi kumuona mwanamume kama Rodriguez.
Mwanamuziki huyo nyota,  alitoa kauli hiyo baada ya wapenzi hao kutembelea familia zote mbili wakati wa mapumziko.
Hii ni mara ya kwanza kwa Jennifer mwenye miaka 48 na Rodriguez (42) kufanya ziara ya kutembelea familia zao.
Mrembo huyo alidokeza Rodriguez ana mapenzi ya kweli na amekuwa akimsaidia katika ‘mambo’ mbalimbali ikiwemo kazi yake ya sanaa.
Katika ziara ya mapumziko Rodriguez aliongozana na watoto wake wawili,
Natasha mwenye miaka 13 na Ella (9) aliozaa na Cynthia Scurtis kati ya mwaka 2002 na 2008.
Rodriguez ‘A-Rod’ ni mchezaji nyota wa zamani wa mpira wa  ‘baseball’ wa klabu ya New York Yankees ya Marekani.
J-Lo aliyekuwa na mama na dada zake wawili na watoto mapacha Max na Emme – aliyezaa na aliyekuwa mumewe Marc Anthony.