Irene Uwoya: Wasanii chipukizi umaarufu hauji kwa kuvaa nguo fupi

Tuesday September 4 2018

 

MWANADADA Irene Uwoya, mtata sana kwani mara kadhaa amekuwa akiingia matatani kwa mashabiki wake kwa kuvaa mavazi tata, lakini sasa msikie alichosema juu ya mavazi hayo kwa sasa.

Mwigizaji huyo amedai umaarufu ni gharama na hauji kirahisi kama watu wanavyofikiria ama kudhani eti huwezi kuwa nyota bila kuvaa nguo nusu utupu, akidai huvaaji wa hivyo haumpendezi hata Mungu na wengi wa mashabiki.

“Kuna wakati lazima wasanii hasa chipukizi watambue umaarufu hauji kwa kuvaa nguo fupi au kashfa, Mungu kwanza hapendi kabisa mtu au msanii kuvaa mavazi ya utupu wafanye kazi ndio watafika mbali,” alisema Irene.

Irene alisema siku hizi usanii umekuwa kutupia picha tata badala ya kuigiza na kuangalia wenye majina njia walizopitia pamoja na urembo lakini walipopewa kazi walifanya vizuri.

Advertisement