Historia yampasua kichwa Shishi baby

MSANII wa kizazi kipya na mjasiriamali, Shilole amesema kinachompasua kichwa ni kutaka kuacha historia miongoni mwa wanawake wa kuigwa duniani na ndio maana hapendi kujibweteka.

Alisema kwa nafasi aliyonayo mbele ya jamii anaamini ana jambo la kufanya litakalokuwa funzo kwa wengine ambao, wanajiona hawawezi kupambana kutafuta kipato chao.

“Wanawake tuna fursa kubwa ya kutafuta kipato katika jamii, ukiachana na muziki ninaofanya ndio maana nimekuwa na sehemu ya chakula.

“Ninachokifanya najua kuna mabinti ambao kitawafunza kwamba, wakijituma na kuwa na malengo wanaweza wakawa na heshima kubwa katika jamii, inawezekana kikubwa wajitume na kujitambua ndio maana napenda kuhamasisha wanawake,” alisema

Alisema Tanzania kuna wanawake wengi wakutazamwa akimtaja Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwamba ni kati ameweza kuongoza nafasi nyeti.

“Wanawake tunaweza wapo wengi katika nafasi mbalimbali, mfano Mama Samia nafasi aliyopo ni kubwa na anachapa kazi,hivyo kila mtu asimame kwa fani ambayo ataiweza,” anasema.