Hiki ndicho kichwa kipya cha Harmonize

Thursday November 15 2018

 

By RHOBI CHACHA

KAMA hujui ni kwamba mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya kutoka Wasafi Classic (Kama ulikuwa unajua kama Mwanamuziki Hamornize  bado meneja wake ni Ricardo Momo,basi jua mambo yamegeuka na kwa sasa amepata meneja mpya.

Hamornize amepata Meneja mpya ambaye anaitwa Joel Vicent Joseph ‘Mr Puaz’,ndiye anayesimamia kazi zake za  Muziki.ambapo Hamornize amewahi kutamba kwenye ngoma ya ‘Aiyola’,’Bado’ aliyomshirikisha Diamond,’Matatizo’,’Sina’,’Ngwangwaru’ na nyingine nyingi.

Baada ya kupata habari hizo,Mwanaspoti lilitinga katika ofisi ya Hamornize iliyopo Sinza Maduka,ambapo ilimkuta Mr Puaz na kufanya nae mahojiano.

Mwanaspoti: Mambo Vipi?

Mr Puaz: Poa tu

Mwanaspoti: Hongereni sana,kwa kuwa Meneja wa Hamornize.

Mr Puaz: Asante sana,tu tunapambana

Mwanaspoti: Umeanza lini kumsimamia Hamornize?

Mr Puaz:Nimeanza kuwa Meneja wa Hamornize ni toka mwezi wa pili,lakini kabla ya hapo mimi nilikuwa rafiki wa Dimond wa muda mrefu, na Hamornize kipindi anataka kutoa wimbo wake Iyola mimi ndiyo nilitengeneza  akaunti ya youtube, na mie ndio nimeweka wimbo wake huo kwenye  Youtube ilikuwa mwaka 2015.

Mwanaspoti:Hivi ilikuwaje hadi ukawa Meneja wa Hamornize ?

MR Puaz :Unajua kama nilivyosema hapo mwanzo, katika urafiki wangu na Diamond,aliweza kunifahamu kupitia vitu vingi sana vya burudani na shughuli mbalimbali, na ilipofika hatua Hamorinize anahitaji Meneja ,alimfata Diamond akamueleza na Diamond akamuelekeza kwangu,naukiangalia Hamornize alikuwa anajua uwezo wangu,hivyo akanipigia simu na kuniambia anatamani tufanye kazi kwa pamoja,hivyo tukakaa chini na kukubaliana na mwisho wa siku tukaanza kufanya kazi mwezi wa tatu na wimbo wa kwa kutoa ilikuwa ni  ‘Ngwangwaru’.

Mwanaspoti:Kabla ya Hamornize,ulishawahi kuwa Meneja wa mwanamuziki yeyote?

Mr Puaz:Ndiyo niliwahi kusimamia wasanii wawili,Hamornize ni msanii wa tatu,wa kwanza alikuwa Shetta mwaka 2014 wimbo na tukifanya wimbo wake wa ‘Namjua’ila kutokana na kubanwa na kazi ambayo niliajiriwa,basi tukaafikiana kuwa aendelee mie nibase kwenye kazi yangu,wa pili alikuwa Ney wa Mitego,huyu alinipa Diamond lakini hatukafanya chochote ikawa tumeishia juu kwa juu.

Mwananspoti:Changamoto gani  unazozipata kumeneji Hamornize,hali yakuwa ni msanii mkubwa sana?

Mr Puaz:Changamoto ni nyingi,moja ukiangalia Hamornize ni msanii na anaangalia vitu katika Levo ya usanii,mimi ni mfanyabiashara na naangalia vitu katika  Levo  biashara,hivyo kuna wakati huwa tunapisha sababu yeye anachukulia kitu kisanii mimi kibiashara,kwahiyo yeye atafanya kitu kwa namna ya kuridhika yeye  kama msanii kuonyesha shoo off, lakini mwisho wa siku ukirudi katika biashara na brand utaona kabisa  hii kitu itaharibu mazingira yetu ya kazi,hivyo lazima tugombane kwenye hivyo vitu na nashukuru ameanza kunielewa.

Mwanaspoti:Nini malengo yako kama Meneja wa Hamornize?

Mr Puaz:Unajua Hamorine ni mtu mwenye kipaji,ana sauti nzuri ukikaa nae ukieleweshana kitu, anakuelewa kwa haraka sana ,japo ubishi upo lakini ni sehemu ya kazi,hivyo malengo yangu Hamornize kumwona anafika levo za wasanii wa kimataifa kama  Justin Bieber, Chris Brown, Usher Raymond na P Diddy.Mtu akiwataja hao na Harmonize asishtuke,na  ili kufia hapo kuna  lazima kutengeneza njia ndefu ya mafanikio.

Mwanaspoti:Hadi sasa kuna mabadiriko gani umeyafanya toka umeanza kumsimamia Hamornize?

Mr Puaz:Kuna vitu vingi nimevibadirisha,kwanza tukianza kwenye mitandao ya kijamii,kuna vitu alikuwa anaposti ambavyo havina maadili ya brand yake posti,kujibizana na watu mitandaoni,hivyo nimemwambia vitu vya kuposti ni kazi zake tu,na naona hilo watu wameona sasahivi wakiangalia akaunti zake za mitandao ya kijamii,na kwenye utendaji wa kazi kwa sasa kuna utofauti ukimuangalia hapo mwanzo alikuwa najiachia achia sana sababu alikuwa free,mambo yake mengi alikuwa anafanya kisanii zaidi,lakini kwakuwa Menejimenti inasimama anakuwa anafanya vitu kibiashara zaidi.

Mwanaspoti:Unameneji Hamornize na Hamornize yuko chini ya WCB kule anakutana na babu Tale,said Fela na salam utofauti wa majukumu ukoje kati ya wale,na ukizingatia watu wengi wanafahamu Meneja wa Hamornize ni Ricardo Momo hii imekaaje?  

Mr Puaz:Hakuna utofauti wowote zaidi ya kukabiziana majukumu,mfano kama Diamond ana Babu Tale,Said Fella na Salam,kwanini anamameneja watatu?kwa sababu kummeneji msanii sio kitu kidogo,hivyo sio mameneja hao hao wanakuwa wanammeneji  Hamornize,Mboso,Ray Vanny,Lava Lava,Qeen Darling,ndio maana mwisho wa siku ikafikia kila mtu atatufe Meneja wake anayeweza kumsimamia kazi zake kwa wanamuziki WCB.

Mwanaspoti:Ni kitu gani unapenda kuona kwa Hamornize akifanya na kipi hupendi?

Mr Puaz:Kitu ambacho sikipendi ubishi na kunihusisha na mambo yake binafsi,na kitu ambacho napenda akifanye ni kukaa studio mara nyingi maana anapenda sana kuzurula zurula.

Mwanaspoti:Asante sana Mr Puazi

Mr Puaz:Nashukuru sana

Advertisement