Harmonize ajisalimisha polisi, anaendelea kushikiliwa

Wednesday February 6 2019

 

By Mwandishi Wetu

Mwanamuziki Harmonize anashikiliwa kwa zaidi ya saa tano katika Kituo cha Polisi Central, jijini Dar es Salaam alipokwenda kujisalimisha akituhumiwa kuvuta kitu kinachofanana na bangi alipokuwa nchini Ghana hivi karibuni.

Akizungumza na wasanii mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema ameagiza mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo Paranawe achunguzwe baada ya  kuweka picha inayomuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.

Makonda alisema alimwagiza Gavana  wa kule amchunguze alichokuwa akivuta na kama ikithibitika kilikuwa na kilevi angemwajibisha.

Makonda ambaye ni mlezi wa lebo ya WCB inayosimamia kazi za Harmonize, alisema kama mzazi angemwajibisha kwa kumweka ndani mwanaye iwapo itathibitika kuwa kilikuwa kilevi.

Leo Februari 6, mwanamuziki huyo alijisalimisha katika kituo hicho  akiwa amejifunika kichwani kwa kuvaa sweta jeusi na miwani.

Alipofika kituoni hapo alitimua mbio huku akiwafurusha waandishi waliokuwa wakijaribu kumpiga picha.

Endelea kufuatilia taarifa hizi hapa....

 

 

Advertisement