Harmonize, Ali Kiba bado mtasubiri sana

Friday July 20 2018

 

MSANII kutoka Lebo ya WCB, Harmonize amefunguka iwapo atakuwa tayari kufanya kolabo na Ali Kiba.

Harmonize amesema hajawahi kutamani kufanya kolabo na msanii huyo na si Ali Kiba pekee, bali na wasanii wengi.

“Lengo la Watanzania wote ni kuona ni kiasi gani tunaweza ku-push muziki wetu na kuupeleka mbali. Sijawahi kutamani kufanya kolabo na Ali Kiba, sijawahi kutamani kufanya kolabo na msanii yeyote lakini ikitokea kipindi tutafanya,” alisema.

“Vitu vingine lazima viwepo ili game izidi kupamba moto, so mimi sidhani kama kuna kitu cha ajabu sana,” alisema Harmonize

Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na kolabo aliyofanya na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwangwaru, huu ni wimbo wa pili kufanya pamoja baada ya ule wa Bado uliotoka mwaka 2016.

Advertisement