Gigy Money ataja kilichombadilisha

Friday April 3 2020

Gigy Money ataja kilichombadilisha,MSANII wa muziki wa bongofleva, Gigy Money ,burudani,mwanasport,

 

By Rhobi Chacha

MSANII wa muziki wa bongofleva, Gigy Money ameibuka na kusema siku zote mtu akiacha utoto, mambo lazima yamnyookee.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gigy alibainisha kuwa mastaa wengi wanapokuwa akili hazijakomaa vizuri, hufanya mambo mengi ambayo siyo sahihi, lakini kuna wakati unafika akili inakomaa, lazima maisha yapige hatua.

“Unajua huko nyuma unaweza usijue kama kuna maisha yanatakiwa yasonge mbele, lakini kama hauko tayari kubadilika kiakili, basi huwezi kusonga mbele.

“Mimi niliacha utoto na kukubali kuwa ni mama Myra, kila kitu kimebadilika.”

Advertisement