Gabo: Wasanii wenzangu wananionea wivu

Monday July 29 2019MSANII wa Filamu nchini, Salim Ahmed 'Gabo'

MSANII wa Filamu nchini, Salim Ahmed 'Gabo' 

By IMANI MAKONGORO

MSANII wa Filamu nchini, Salim Ahmed 'Gabo' amesema wasanii wenzake wamekuwa wakimuonea wivu.
Gabo ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Tecno amesema tangu amepata nafasi hiyo amejitofautisha na wasanii wengine.
Msanii huyo alibainisha hayo wakati wa uzinduzi wa simu ya Tecno Phantom 9 ambayo imeanza kuuzwa kwa oda maalumu nchini.
"Kabla ya uzinduzi huu, mabosi wangu walileta simu za Phantom 9 tatu pekee nchini, ambayo moja ni ya hii ya kwangu," alisema Gabo na kuendelea.
"Kwa huduma ambazo ziko kwenye hii simu, wasanii wenzangu kila nilipokwenda walinionea wivu, lakini bahati mbaya hawakuwa na uwezo wa kuipata hivyo kwani hazikuwepo nchini," alisema.
Alisema alijitofautisha nao ingawa sasa Tecno imeamua kuleta Phantom 9 kwa oda maalumu.
Meneja uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye amesema Gabo amekuwa balozi wao wa tofauti na kusisitiza kuwa ujio wa Phantom 9 utarahisha mambo mbalimbali kwa watumiaji ikiwamo wasanii.

Advertisement