Fid Q hajapoteza kitu buana!

Muktasari:

  • Mwanaspoti ilifanya mahojiano na mkali huyo na kufunguka ikiwamo ishu yake ya ndoa.

ZANZIBAR.LICHA ya mashabiki wa muziki kupata burudani toka vikundi vya Wamwiduka, S Kide na Damian Solo waliopiga muziki wao laivu, mkali wa hip hop Fid Q naye alikonga nyoyo za waliojitokeza kwenye Tamasha la 16 la Sauti za Busara 2019, linalomalizika jana Jumapili visiwani hapa.

Fid Q alionyesha kupevuka kisanii kutokana na kuimba muziki wake ‘live’ na kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika Viwanja vya Ngome Kongwe mwishoni mwa wiki hii.

Staa huyo wa Fresh, alipanda jukwaani saa 4:00 usiku akiimba wimbo wa Chagua Moja kisha kuangusha moja moja kama Mwanza, Sihitaji Marafiki na Dot Com. Pia aliimba nyimbo zake nyingine kama Ripoti za Mtaani, Propaganda, Sumu, Siri ya Mchezo, Maisha ya Jela na Fresh.

Mkali huyo aliyeanza fani miaka ya 1990 akitambuliwa na Huyu na Yule wa mwaka 2000 alioimba na Mr Paul.

Mwanaspoti ilifanya mahojiano na mkali huyo na kufunguka ikiwamo ishu yake ya ndoa.

“Naweza kusema nina bahati na kujituma katika kufahamu umuhimu wa Tamasha la Sauti za Busara, kwanza hii ni mara ya sita kushiriki katika tamasha hili, ninayependa kujifunza zaidi ndio maana nashiriki kila mara,” alisema.

“Unapoimba laivu kuna raha yake kwanza inasaidia kusikia vizuri pia unapata mashabiki wengi kutokana na ujumbe unaotoka kusikia vizuri.”

Mkali huyo aliwashauri wasanii wenzake hasa chipukizi kujenga utamaduni wa kuimba muziki hai, ili kuonyesha uwezo wao na na kupenda kujifunza kwa watu wengine wanaofanya kazi kama hiyo.

“Tatizo ni Watanzania hawapendi wala kuuthamini utamaduni watu. Kinachosikitisha, tamasha kama hili kubwa Afrika, wamejaa wazungu, wanapenda utamaduni wao na hata wapo tayari kujifunza juu ya utamaduni wa watu wengine,”

kuhusu maisha ya ndio alisme: “Kiukweli maisha ya ndoa niseme tu nafurahishwa nayo na najiona kama nimechelewa.”