Ebwana! Kumbe Lulu Simba damu, awatumia salamu Al Ahly

Monday February 11 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Movie amesema, yeye ni shabiki mkubwa wa Klabu ya Simba na anaamini itamchapa Mwarabu wa Al Ahly ya Misri kesho Jumanne Uwanja wa Taifa.

Simba klabu pekee ukanda wa Afrika Mashariki imevuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na katika michuano hiyo wamepangwa pamoja na timu za JS Saoura ya Algeria, Al Ahly ya Misri na AS Vita ya Congo.

Lulu ambaye yuko katika kampeni za Save My Valentine ambazo inawahusu zaidi wahitaji amesema, aliipenda klabu hiyo kwa sababu ya mama yake mzazi,  Lucresia Karugila.

"Mama yangu ni shabiki wa Simba hivyo na mimi nikajikuta naipenda tu klabu hii. Ulikuwa ni mkumbo tu lakini mwisho wa siku mapenzi yakawa ndiyo kama hivyo,"alisema Lulu ambaye hivi karibuni alivalishwa pete ya uchumba na mmliki wa kituo cha radio na terevisheni, Francis Ciza 'Majizzo'.

"Sifatilii sana mpira lakini naamini Simba wataifunga Al Ahly katika mchezo wao wa kesho, nawaombea na nawapenda."

Advertisement