Dua maalum yaandaliwa kumuombea mama wa P funk

Saturday September 19 2020

 

By KELVIN KAGAMBO

Dua maalum ya kumtakia rehema mama mzazi wa prodyuza wa muziki wa kizai kipya, P Funk ambaye alifariki Sepetemba 8 inafanyika leo mchana jijini Dar es Salaam.

Msimamizi tukio hilo ambaye pia ni mpwa wa marehemu, Fadhil Kiholi amesema dua hiyo itafanyika saa saba mchana baada ya sala ya adhuhurI, kisha familia itakaa kikao kwa ajili ya kujadili mipango mingine ikiwemo ya arobaini.

"Tulishamzika shangazi Uholanzi,kwahiyo hapa tunafanya dua tu. Itakuwa saa saba mchana na baada ya dua hiyo familia tutakaa kujadili kuhusu wapi arobaini ifanyike kati ya Dar es Salaam au Morogoro."

Mama P Funk ambaye jina lake maarufu ni Aunt Sheilah alifariki Septemba 8 nchini Uholanzi alipokuwa akipatiwa matibabu, lakini baada ya mipango na kumsafirisha kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi kushindikana familia iliamua kumzika huko huko.

Pia Fadhili ameongeza kuwa ndugu zote waliokuwa kwenye mazishi Uholanzi wamerudi na watahudhuria dua ya leo akiwemo P Funk mwenyewe.

Advertisement